WATUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA WAZIDI KUBANWA

WATUHUMIWA DAWA ZA KULEVYA WAZIDI KUBANWA

Like
315
0
Monday, 11 April 2016
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.

 

Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza hilo, hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.

 

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wilayani Ruangwa wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi.

Comments are closed.