WATUHUMIWA WA UNYANG’ANYI KWA KUTUMIA SILAHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

WATUHUMIWA WA UNYANG’ANYI KWA KUTUMIA SILAHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Like
261
0
Thursday, 15 January 2015
Local News

                                              

JUMANNE JULIUS mwenye umri wa miaka 21 na JAFARI DIOMBA mwenye umri wa miaka 20 wakazi wa jijini Dar es salaam wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya kinondoni jana kwakosa la unyanganyi kwa kutumia silaha.

Wakisomea shitaka hilo mbele ya hakimu IZ-HAQ KUPPA na mwendesha mashitaka MAGOMA MTANI amesema kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Novemba 16 mwaka jana maeneo ya mbezi beach wilaya ya kinondoni.

Mtani amebainisha kuwa washitakiwa hao kabla na baada ya wizi walimtishia kwa bastola na kufanikiwa kuiba simu aina ya Samsang S4 yenye thamani ya shilling laki tano, Black berry carve yenye thamani ya shilingi laki nne na nusu pamoja na computa mpakato –laptop yenye thamani ya shilingi laki sita na nusu ikiwa ni mali ya MOHAMED HASSAN.

 

Comments are closed.