WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WATAKIWA KUHUDUMIA WANANCHI

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WATAKIWA KUHUDUMIA WANANCHI

Like
306
0
Tuesday, 24 November 2015
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo.

 

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa Taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.

 

Mbali na hayo amewataka watumishi hao kuwa tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais dokta John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi wa Serikali.

Comments are closed.