WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WAMETAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WAMETAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

Like
197
0
Wednesday, 16 December 2015
Local News

SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa.

 

Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.

 

Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza kwa bidii ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2015.

 

Comments are closed.