WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUVAA BEJI ZA KUWATAMBULISHA

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUVAA BEJI ZA KUWATAMBULISHA

Like
281
0
Wednesday, 02 December 2015
Local News

KATIBU MKUU Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa  katika maeneo  ya  kazi.

Balozi Sefue ametoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine.

Amesema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza  watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao.

Comments are closed.