WAUZAJI wa mboga mboga na matunda waliopo karibu na soko la Mjini Babati Mkoani Manyara, ambao wanauza bidhaa zao chini wametoa ombi kwa halmashauri ya mji huo kumalizia ujenzi wa soko jipya ili waweze kuhamishia bidhaa zao hapo.
Wakizungumza wakati mwenge wa uhuru ukiweka jiwe la msingi kwenye soko jipya, wafanyabiashara hao wamedai wanakuwa na wakati mgumu kwani soko la sasa ni dogo na halitoshelezi mahitaji.
Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela, amemweleza kiongozi wa mbio za mwenge, Juma Khatib Chum kuwa tayari amekwisha mwagiza mkurugenzi wa mji huo Omary Mkombole kuhakikisha wanatenda haki katika kugawa eneo hilo.