Wavulana 4 zaidi waliokwama pangoni Thailand 'waokolewa'

Wavulana 4 zaidi waliokwama pangoni Thailand 'waokolewa'

Like
658
0
Tuesday, 10 July 2018
Global News

 

Wapigaji mbizi kaskazini mwa Thailand wamewaokoa wavulana
wanne zaidi kutoka pango lililofurika maji.
Hii inaashiria kuwa kwa jumla, wavulana 8 wameokolewa salama
huku watu watano wakiwa bado wamesalia ndani ya pango.
Vijana hao 12 na kocha wao wa soka walikwama ndani ya pango
tangu Juni 23 baada ya mvua kubwa kusababihsa mafuriko.
Wanajeshi wa majini wa Thailand wanaoongoza operesheni hiyo
wamethibitisha kuwa jumla ya wavulana 8 wameokoloewa salama.
Wavulana 4 waliokolewa salama kutoka pangoni siku ya Jumapili.
Lakini operasheni hiyo ilisitishwa usiku ili mitungi ya hewa ya
kusaidia kupumua ipate kujazwa.
Wakoaji waliamua kuendelea na oparesheni hiyo hatari kuwaokoa
kufuatia hofu kuwa huenda maji yangeongezeka tena.
Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani ya
pango hilo,ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kazi hiyo inaharakishwa kufuatia utabiri wa hali ya hewa unaodai
kwamba huenda mvua kubwa itanyesha jambo ambalo litasababisha
ugumu wa kazi ya kuwaokoa watoto hao.
Kiongozi wa kikosi cha uokoaji ambaye gavana wa jimbo la Chang
Raiu Narongsak Osottanakorn, amesema uokoaji huo wenye
mazingira ya hatari utawachukua takribani siku nne kutegemeana
na hali ya hewa, japo kuwa jana kwamba amesisitiza kila kitu
kinaenda sawa.

Warembo 16 katika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *