WAYAHUDI WENYE MSIMAMO MKALI WAYACHOMA MOTO MAKAZI YA WAPALESTINA

WAYAHUDI WENYE MSIMAMO MKALI WAYACHOMA MOTO MAKAZI YA WAPALESTINA

Like
236
0
Friday, 31 July 2015
Global News

WATU wanaoshukiwa kuwa ni Wayahudi wenye msimamo mkali wameyachoma moto makazi ya Wapalestina huko Ukingo wa Magharaibi hii leo na kumuua mtoto wa miezi 18 na kuwajeruhi wengine wanne.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyaita mashambulizi hayo kuwa ni tukio la kigaidi na kusema kuwa ameshitushwa na kitendo hicho cha kinyama ambacho kina dhamira zote za kigaidi.

Msemaji wa Serikali ya Israel Mark Regev amesema wanahakikisha wanawakamata na kuwashitaki waliohusika katika tukio hilo huku wazazi wa mtoto huyo aliyeuawa pamoja na kaka yake wa miaka minne wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo.

Comments are closed.