WAZAZI nchini wameshauriwa kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo hasa kwa baadhi ya shule za msingi nchini.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mtabibu wa tiba mbadala Abdalah Mandai wakati akizungumza na kituo hiki juu ya changamoto mbalimbali za sekta ya elimu nchini.
Amesema kuwa baadhi ya shule za msingi zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati pamoja na vyumba vya madasara kitendo kinachochangia wanafunzi kusoma huku wakiwa wamekaa chini na hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya mtoto.