UKOSEFU wa Damu katika hospital mbalimbali nchini unaweza kusababisha madhara makubwa,ikiwemo vifo vya Kinamama na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Hayo yamesema na Shirika lisilo la kiresikali linalojishughulisha na masuala ya Afya la SIKIKA katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wa damu.
Mkurugenzi wa SIKIKA IRENE KIWIA,amesema kuwa upungufu wa damu uliotangazwa na Mpango wa taifa wa damu salamu-NBTS,unapaswa kushughulikiwa ipavyo ili kuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa kinamama na watoto.