WAZAZI nchini wameshauriwa kujenga utamaduni wa kuwawekea watoto wao bima za elimu ili ziweze kuwasaidia kutimiza ndoto zao badala yakusoma huku wakiwa na wasiwasi wa karo na kufukuzwa shule.
Wito huo umetolewa leo na Afisa mipango fedha kutoka kampuni ya Alliance life Assurance ambayo inayojishughulisha na masuala ya bima ya maisha na elimu, ANNY MUSHI ambaye amesema kuwa endapo familia zitakuwa na mwamko wakuwekea watoto wao bima ya elimu kuna uwezekano mkubwa familia nyingi zikamudu gharama za elimu nchini.