WAZAZI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kudharau mikakati mbalimbali ya serikali kuhusu afya za watoto na badala yake wawapeleke kupata chanjo na kuchunguza afya zao.
Aidha wazazi pia wametakiwa kuwapeleka watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 katika zahanati na vituo mbalimbali vya afya kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha akina mama na watoto wa zahanati ya Arafa Ugweno iliyopo Tandika jijini Dar es salaam Latifa Masasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Zoezi hilo.