WAZEE CHADEMA WATOA TAMKO KUFUATIA MAAMUZI YA KINGUNGE

WAZEE CHADEMA WATOA TAMKO KUFUATIA MAAMUZI YA KINGUNGE

Like
434
0
Thursday, 08 October 2015
Local News

BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA limesema kuwa uamuzi wa Mwanasiasa nguli Nchini Kingunge Ngombale Mwiru kujitoa katika Chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa CCM inahitaji mabadiliko ya mfumo ni ishara kuwa Taifa linahitaji mabadiliko ya ukweli na ya uhakika.

 

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Katibu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Roderick Rutembeka amesema kuwa Mwanasiasa mkongwe huyo ameweza kuwatoa hofu Watanzania wote kuwa mabadiliko sio jambo geni nchini na kwamba kumekuwa na mabadiliko ya kisiasa mbalimbali tangu uhuru wa Tanzania.

Comments are closed.