WAZEE WAIOMBA SERIKALI IJAYO KUZINGATIA MAHITAJI MUHIMU

WAZEE WAIOMBA SERIKALI IJAYO KUZINGATIA MAHITAJI MUHIMU

Like
263
0
Thursday, 01 October 2015
Local News

KATIKA kuadhimisha siku ya wazee dunia leo, baadhi ya wazee waishio jijini dar es Salaam wameiomba serikali ijayo kuhakikisha inazingatia mahitaji muhimu ya wazee nchini ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi ya huduma bure za matibabu.

Wakizungumza na kituo hiki wazee hao wameeleza kuwa ahadi ya huduma bure za afya haijaweza kutekelezeka kwani wazee wengi wakienda kupata matibabu katika hospitali za serikali wanatibiwa magonjwa madogomadogo na yale yanayohitaji vipimo vikubwa na dawa wanatakiwa kujihudumia wenyewe.

Comments are closed.