WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

Like
324
0
Thursday, 03 March 2016
Local News

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao za kuisaidia serikali.

 

Makamba ametoa wito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam.

 

Makamba amesema kamati hiyo ni muhimu katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe wa kamati hiyo na wananchi kwa ujumla.

Comments are closed.