WAZIRI MAGEMBE AZINDUA RASMI RIPOTI YA UTENDAJI WA MAMLAKA ZA MAJI

WAZIRI MAGEMBE AZINDUA RASMI RIPOTI YA UTENDAJI WA MAMLAKA ZA MAJI

Like
307
0
Friday, 19 December 2014
Local News

WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amewataka wamiliki wote wa Viwanda nchini kutotupa ovyo taka zisizo tibiwa kwa dawa kwenye mito ya maji ili kupunguza athari zitokanazo na tatizo hilo kwa binadamu.

Profesa Maghembe ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua rasmi ripoti ya utendaji wa Mamlaka za maji za Mikoa na miradi ya maji ya Kitaifa ya mwaka 2013-2014, kwa lengo la kuboresha huduma za maji nchini.

Katika uzinduzi huo pia amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji nchini inaendelea kuboreka maeneo mbalimbali nchini.

Comments are closed.