WAZIRI MKUU AFUNGUA TAWI LA BENKI YA POSTA SONGEA

WAZIRI MKUU AFUNGUA TAWI LA BENKI YA POSTA SONGEA

Like
420
0
Tuesday, 05 January 2016
Local News

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua tawi la Benki ya Posta iliyopo mjini Songea, wakati akiwa katika ziara mkoni Ruvuma inayotarajiwa kumalizika kesho, jumatano.

 

Akizungumza  na uongozi  na wafanyakazi wa  Benki ya Posta pamoja na wateja waliohudhuria ufunguzi  wa tawi hilo uliofanyika  nje ya benki hiyo, Waziri Mkuu  amesema amefarijika kuona benki hiyo  iliyokua imekumbwa na matatizo sasa imezaliwa upya na kumpongeza Mkurugenzi wa Benki ya Posta  nchini Bwana. Sabasaba Mushindi kwa jitihada zake za kuifufua.

D2

 

Comments are closed.