WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA TUMBAKU MKOANI RUVUMA

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA TUMBAKU MKOANI RUVUMA

Like
303
0
Wednesday, 06 January 2016
Local News

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika  tumbaku  cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.

 

Alikuwa akizungumza  katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.

 

Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.

Comments are closed.