Waziri Mkuu azitaka taasisi za dini kuwekeza kwenye viwanda

Waziri Mkuu azitaka taasisi za dini kuwekeza kwenye viwanda

Like
429
0
Thursday, 12 July 2018
Local News

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini wasibaki nyuma katika suala zima la kuwekeza kwenye viwanda ili waweze kuendana na azma ya Serikali ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi wa viwanda. Nawaomba msiwe nyuma katika suala hili, tumieni fursa ya ardhi tuliyonayo hasa katika ujenzi wa viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo Alhamisi, Julai 12, 2018 wakati akifungua mkutano wa halmashauri kuu ya 52 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *