WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA KAMATI YA UCHUMI BARIADI IKUTANE NA WAFANYABIASHARA KUPANGA USHURU

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA KAMATI YA UCHUMI BARIADI IKUTANE NA WAFANYABIASHARA KUPANGA USHURU

Like
352
0
Friday, 04 March 2016
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo.

 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

 

Waziri mkuu Majaliwa mefikia uamuzi huo baada ya kuona bango lililoshikwa na wananchi wakilalamikia kutozwa ushuru wa shilingi Elfu 3 kwa gunia moja la mazao badala ya shilingi Elfu moja ya zamani.

Comments are closed.