WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA WITO HUU KWA WATAALAMU WA UHIFADHI WA URITHI ASILIA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA WITO HUU KWA WATAALAMU WA UHIFADHI WA URITHI ASILIA

Like
299
0
Tuesday, 31 May 2016
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa mambo ya malikale na uhifadhi wa urithi asilia watafute mbinu zitakazoimarisha utunzaji wa rasilmali hizo bila kuathiri mifumo ya uchumi wa nchi zinazoendelea.

 

Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito huo leo Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa siku nne unaojadili Uhifadhi wa Urithi wa Dunia wa Afrika kama Nyenzo ya kuleta Maendeleo Endelevu.

 

Waziri Mkuu amesema endapo rasilmali hizo zitachambuliwa vizuri na kwa njia sahihi bila kuathiri vivutio vya urithi wa dunia, ni dhahiri kuwa zitaingiza mapato ambayo kiuchumi yatasaidia kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi.

 

Comments are closed.