WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUMUWAKILISHA RAIS UINGEREA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUMUWAKILISHA RAIS UINGEREA

Like
911
0
Tuesday, 10 May 2016
Local News

WAZIRI mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa anaenda kumuwakilisha Mheshimiwa Rais kwa sababu siku hiyo ya mkutano atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yower Museven

 

Akizungumzia kuhusu suala la kupambana na rushwa waziri Mkuu amesema kuwa Tanzania inafanya jitihada kubwa katika mapambano dhidi ya Rushwa hali inayoanza kuzivutia nchi nyingine.

Comments are closed.