WAZIRI MKUU KUZITEMBELEA KAYA 145 ZILIZOATHIRIWA NA MAFURIKO IRINGA

WAZIRI MKUU KUZITEMBELEA KAYA 145 ZILIZOATHIRIWA NA MAFURIKO IRINGA

Like
318
0
Monday, 22 February 2016
Local News

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, leo anatarajia kuzitembelea kaya zaidi ya 145 zilizoathiriwa na mafuriko katika kata ya Pawaga, wilayani Iringa kwa lengo la kuzifariji.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu anatarajiwa kuambatana na Mbunge wa Jimbo la Isimani ilipo kata hiyo, William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambao kwa pamoja watajionea hali halisi ya maisha ya kaya hizo zinazoendelea kusaidiwa ili zirudi katika maisha yake ya kawaida.

Hata hivo mkuu wa wilaya ya Iringa, Bwana Richard kasesela amewaomba wadau na wasamalia wema kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula huku akisema kwa sasa zinahitajika nyumba za haraka 58 kwa ajili ya wahanga hao.

Comments are closed.