WAZIRI mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras anazidi kukabiliwa na upinzani huko Athens kwa hatua mpya na kali za malipo alizokubali kuzitambulisha kutokana na masharti mapya ya kuokoa kuporomoka kwa uchumi.
Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Panos Kammenos ambaye anaongoza chama kidogo katika muungano wa serikali ya kitaifa ameelezea mpango huo kuwa ni mapinduzi ya serikali.
Habari kutoka chama hicho zinasema kwamba mkataba uliowekwa ni wa kuifedhehesha Ugiriki nchi hiyo kwa kuwa unalitaka bunge la ugiriki kupitisha ongezeko la kodi, kupunguza mafao na kufanya mabadiliko ya sheria ya ajira ifikapo siku ya jumatano.