WAZIRI MKUU wa Serikali ya Libya inayotambulika kimataifa, Abdullah al-Thani amejiuzulu katika hatua ya kushangaza jana, saa chache baada ya mazungumzo ya amani kati ya makundi hasimu ya nchi hiyo kuanza.
Wakati wa kipindi cha mazungumzo katika televisheni kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja, waziri mkuu Al-Thani alipambana na maswali makali ya watu wenye hasira ambao wameilaumu serikali yake kwa kushindwa kutoa huduma muhimu kama umeme na usalama katika maeneo inayoyadhibiti.