WAZIRI MKUU WA LIBYA AJIUZULU

WAZIRI MKUU WA LIBYA AJIUZULU

Like
162
0
Wednesday, 12 August 2015
Slider

WAZIRI MKUU wa Serikali  ya  Libya  inayotambulika kimataifa, Abdullah al-Thani  amejiuzulu  katika  hatua  ya kushangaza jana, saa  chache  baada  ya  mazungumzo ya  amani  kati  ya  makundi  hasimu  ya  nchi  hiyo kuanza.

 

Wakati  wa  kipindi  cha  mazungumzo  katika  televisheni kilichokuwa  kikirushwa  moja  kwa  moja, waziri  mkuu Al-Thani  alipambana na maswali  makali  ya  watu  wenye hasira ambao  wameilaumu  serikali  yake kwa  kushindwa kutoa huduma  muhimu kama  umeme  na  usalama  katika maeneo  inayoyadhibiti.

 

Comments are closed.