WAZIRI MKUU mpya wa Ugiriki Alexis Tsipras anaendelea na ziara ya mataifa ya Ulaya tangu aingie madaraka wiki moja iliyopita, katika jitihada za kutafuta kuungwa mkono mpango wa kutaka suala la kuiokoa nchi yake na mzigo wa madeni lijadiliwe upya.
Anakwenda Italia leo kwa mazungumzo na waziri mkuu Matteo Renzi.
Jana waziri mkuu huyo aliondoa uwezekano wa kufanyakazi pamoja na kundi la pande tatu la wakopeshaji wa kimataifa.