WAZIRI MKUU WA UGIRIKI AWASILI MOSCOW KUFANYA MAZUNGUMZO MAALUM

WAZIRI MKUU WA UGIRIKI AWASILI MOSCOW KUFANYA MAZUNGUMZO MAALUM

Like
245
0
Wednesday, 08 April 2015
Global News

WAZIRI Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, amewasili mjini Moscow kukutana rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mazungumzo maalum.

Ugiriki inasema kuwa mazungumzo yao yatajadili uhusiano kati ya muungano wa bara la Ulaya na Urusi.

Uhusiano huo ulidorora kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni kufuatia mzozo wa Ukraine.

Wachanganuzi wanasema kuwa Ugiriki inapania kuboresha uhusiano na Moscow hasa ikiwa uhusiano wao na wadeni wao bara Ulaya wa kuikopesha pesa ukishindikana ambapo kesho nchi hiyo inatakiwa kulipa deni la dola milioni 886 kwa shirika la fedha duniani IMF.

 

Comments are closed.