WAZIRI MWAKYEMBE AWAONYA MAOFISA HABARI WA SERIKALI

WAZIRI MWAKYEMBE AWAONYA MAOFISA HABARI WA SERIKALI

Like
340
0
Tuesday, 13 March 2018
Local News

 

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr. Harison Mwakyembe amewaonya maofisa habari wa serikali ambao hawatangazi kazi za maendeleo zinazofanywa na serikali watachukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi.

Dr. Mwakyembe ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wananchama wa chama cha maafisa mahusiano serikalini unaofanyika mkoani Arusha, nakusema maafisa habari wa serikali ambao wanatumia vifaa walivyopewa kwa matumizi yao binafsi pamoja na wale wanaokaa maofisini bila kufanya kazi nakusubiri muda wakutoka.

Kwa upande wa msemaji wa serikali Dr. Hassan Abas amesema wataanza kuwapima maafisa habari kutokana na utendaji wao na tayari wameweka maelengo saba ikiwemo kujibu kero za kwenye mitandao ikiwemo twitter,instagram na facebook.

Comments are closed.