WAZIRI MWIJAGE AKALIWA KOONI

WAZIRI MWIJAGE AKALIWA KOONI

Like
266
0
Wednesday, 19 October 2016
Slider

Dodoma. Vuta nikuvute iliibuka jana kwenye Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira baada ya wajumbe wake kuikataa taarifa ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhusu utekelezaji wa malengo ya sekta ya viwanda na biashara, wakidai imejaa porojo.

Hali hiyo ilisababisha mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Dalali Kafumu kuwaondoa ukumbini Waziri, Katibu na wataalamu waliofika hapo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi na kujibu maswali ya wabunge.

Taarifa ya maandishi ya utekelezaji wa malengo ya sekta ya viwanda na biashara ya Julai 2016 hadi Oktoba 2016, ilikuwa tayari imekabidhiwa kwa wabunge siku chache kabla ya kikao hicho.

Comments are closed.