WAZIRI NAPE AZINDUA RASMI KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA

WAZIRI NAPE AZINDUA RASMI KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA

Like
274
0
Friday, 01 April 2016
Local News

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua rasmi kamati ya maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA itakayoangalia maudhui bora ya utangazaji wa vipindi na matangazo katika vyombo vya habari nchini.

 

Aidha, ameitaka taka kamati hiyo kuangalia suala la baadhi ya Watu kushikilia masafa mengi bila ya kutumia pamoja na kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri kanuni za utangazaji ziweze kufuatwa na kuheshimiwa ipasavyo.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya Mamlaka ya mawasiliano Profesa Semboja Haji amesema jukumu muhimu la kamati hiyo ni kuhakikisha kuwa vituo vyote vya habari vinatumia maudhui bora katika kurusha vipindi na matangazo yao .

Comments are closed.