WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA KAIMU AFISA BIASHARA WA MANISPAA YA ILALA

WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA KAIMU AFISA BIASHARA WA MANISPAA YA ILALA

Like
415
0
Thursday, 07 January 2016
Local News

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa, George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala  Dennis Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.

 

Kutokana na hali hiyo Waziri ameelekeza Mkurugenzi huyo wa Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

Comments are closed.