WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA TAASISI YA BASILLA MWANUKUZI BMF

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA TAASISI YA BASILLA MWANUKUZI BMF

Like
263
0
Monday, 11 April 2016
Local News

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu leo amezindua rasmi taasisi ya Basilla Mwanukuzi BMF-yenye lengo la kushirikiana na Wadau ili kuwawezesha Wanawake kiuchumi.

Hafla hiyo ya uzinduzi imeenda sanjari na uzinduzi wa mradi wa “Wezesha mama lishe Tanzania” ukiwa na lengo la kuwawezesha mama lishe kupata elimu ya ujasiriamali na upikaji wa chakula bora chenye kuzingatia virutubisho.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mwalimu amesema kuwa wengi waliopo katika sekta ya mama lishe ni Wanawake na ni wazi kuwa kumwezesha Mwanamke ni kuiwezesha familia Jamii na Taifa kwa ujumla.

Comments are closed.