WAZIRI WA ARDHI AELEZA UMUHIMU WA KUPANGA MAENEO YA MAKAZI

WAZIRI WA ARDHI AELEZA UMUHIMU WA KUPANGA MAENEO YA MAKAZI

Like
285
0
Monday, 05 October 2015
Global News

NAIBU waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa ANGELLAH KAIRUKI amesema kuwa ni lazima kuweka umuhimu mkubwa katika kupanga, kutenga, kupima, kuendeleza na kusimamia maeneo ya Umma kwa kuzingatia sheria na mahitaji maalum na salama kwa watumiaji wakiwemo wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Kairuki ameiambia EFM leo kwenye maadhimisho ya siku ya makazi duniani yaliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa ili kuhakikisha uwepo wa utumiaji salama wa maeneo ya umma hususani sehemu za ardhi ambazo zipo wazi juhudi za dhati zinatakiwa katika kupanga na kusimamia uendelezaji ardhi hizo kwa kuzingatia utawala bora na uongozi imara wa miji wenye kufuata sera za matumizi sahihi ya ardhi zilizowekwa na serikali

Comments are closed.