WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI

Like
241
0
Monday, 14 December 2015
Local News

WAZIRI  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameahidi kushirikiana na Waandishi wa habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya habari Nchini.

 

Waziri Nape ameyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo alipoingia Wizarani hapo kuanza kazi rasmi ambapo amesema amekusudia kuwa mlezi wa wanahabari pamoja na vyombo vya habari huku akimtaka kila mtu katika tasnia hiyo kutekeleza wajibu wake kwa kufuata misingi na utaratibu na kazi.

Comments are closed.