WAZIRI wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani FRANK-WALTER STEINMEIER amewasili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Kituo cha kwanza cha ziara yake ya siku nne barani Afrika.
Kabla ya ziara hiyo kuanza,Mwanasiasa huyo kutoka Chama Cha Social Democratic amesema, uhusiano wa siku za mbele pamoja na Bara la Afrika amesema utatuwama katika juhudi za kuepusha Mizozo,Ushirikiano katika masuala jumla na Ushirikiano wa kiuchumi.
Mbali na Jamhuri Kidemokrasia ya Kongo,Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani amepanga kuzitembelea pia Rwanda na baadae Kenya.
Katika ziara yake hiyo barani Afrika Waziri huyo amefatana na ujumbe wa Kibiashara na Kitamaduni.