WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ITALY AWASILI LIBYA

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ITALY AWASILI LIBYA

Like
276
0
Tuesday, 12 April 2016
Global News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Italia amewasili mjini Tripoli Libya, kwa mazungumzo na kiongozi wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya Fayez Seraj.

Paolo Gentiloni ni afisa mkuu wa kwanza wa bara la Ulaya kufanya ziara rasmi nchini Libya tangu utawala mpya unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kuwekwa katika mji mkuu wa Libya majuma mawili yaliyopita.

Italia pamoja na mataifa kadhaa ya dola za kimagharibi yaliyoitawala Libya miaka iliyopita yameahidi kuisaidia serikali hiyo mpya kwa imani kuwa italeta umoja wa kitaifa na kuwaunganisha raia dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Islamic State.

Comments are closed.