WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI AONYA KUSAMBAA KWA MZOZO UKRAINE

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI AONYA KUSAMBAA KWA MZOZO UKRAINE

Like
238
0
Tuesday, 24 March 2015
Global News

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, FRANK-WALTER STEINMEIER amesema pande zinazohusika katika mzozo wa Ukraine, lazima ziepukane na hatua zozote zinazoweza kupelekea mzozo mpya kusambaa zaidi nchini humo.

Aidha, STEINMEIER ametoa wito wa kuendelea kwa mchakato wa mpango wa amani wa Minsk, ambao umesainiwa mwaka uliopita, katika juhudi za kusimamisha mapigano Mashariki mwa Ukraine.

STEINMEIER na maafisa wengine waandamizi wanaohusika na mzozo wa Ukraine, wanatarajiwa kukutana mjini Paris, Ufaransa kujadiliana kuhusu hatua za kusitisha mapigano Ukraine.

Comments are closed.