WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI AWAALIKA MAWAZIRI WENZAKE BERLIN KUJADILI MAKUBALIANO YA AMANI UKRAINE

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI AWAALIKA MAWAZIRI WENZAKE BERLIN KUJADILI MAKUBALIANO YA AMANI UKRAINE

Like
223
0
Friday, 10 April 2015
Global News

WAZIRI wa Mambo ya  Nje wa Ujerumani  Frank – Walter Steinmeier  amewaalika  Mawaziri  wenzake   kutoka  Urusi, Ukraine na  Ufaransa  mjini  Berlin  siku  ya  Jumatatu  kujadili utekelezaji  wa makubaliano  ya  amani  yaliyofikiwa  mjini  Minsk  kuhusu  mashariki mwa  Ukraine, nchini  Belarus Februari mwaka  huu.

Mzozo  kati ya waasi wanaoungwa  mkono  na  Urusi  na  Majeshi ya  Serikali  ya  Ukraine  mashariki mwa nchi hiyo umesababisha watu elfu sita kupoteza  maisha.

Viongozi  wa  Ujerumani na  Ufaransa  wamesimamia  upatikanaji  wa makubaliano  ya  kusitisha  mapigano  mjini  Minsk  katika  juhudi  za kusitisha  umwagikaji  wa  damu , na  uhasama  umepungua  licha  ya kuwa  tofauti  bado  zipo katika  kupiga  hatua.

 

Comments are closed.