WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI

WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI

Like
198
0
Thursday, 31 March 2016
Global News

WAZIRI wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.

 

Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua.

 

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.

Comments are closed.