WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AANZA KAZI RASMI

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AANZA KAZI RASMI

Like
224
0
Tuesday, 15 December 2015
Local News

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, dokta Hussein Mwinyi, aliyeteuliwa na kisha kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu ameripoti ofisini na kuanza kazi rasmi.

 

Waziri Mwinyi amewasili ofisini kwake na kulakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Majeshi Mnadhimu Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, wanajeshi na watumishi wa Umma wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Job Masima.

 

Akizungumza na Menejimenti ya Wizara, Waziri Mwinyi amesema matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza ufanisi, kupunguza urasimu pamoja na kupunguza matumizi ya serikali pasipo kuathiri utendaji kazi.

Comments are closed.