WAZIRI WA USALAMA AWAOMBA RADHI WANAFUNZI KENYA

WAZIRI WA USALAMA AWAOMBA RADHI WANAFUNZI KENYA

Like
429
0
Tuesday, 20 January 2015
Global News

WAZIRI wa Usalama Nchini Kenya Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.

wana

Bwana Nkaissery amempa Mvamizi wa ardhi hiyo siku moja kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo.

Ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hiyo na kuiacha kuwa uwanja wa kuchezea wanafunzi hao.

Comments are closed.