WEASEL KUKAMILISHA NDOTO YA MKEWE KWAKUMJENGEA NYUMBA MKWE WAKE

WEASEL KUKAMILISHA NDOTO YA MKEWE KWAKUMJENGEA NYUMBA MKWE WAKE

Like
444
0
Friday, 31 July 2015
Entertanment

Mama mzazi wa Samira ambae ni mpenzi wa muimbaji Weasel kutoka Uganda huenda akawa kwenye list ya wazazi wanaojivunia kuwa na watoto wa kike wanaowajali na kuwafanikishia ndoto zao.

Hili linakuja mara baada ya mchumba huyo wa mwimbaji Weasel kuwekewa masharti iwapo atahitaji kumuoa mrembo huyo basi moja ya vitu vikubwa atakavyolazimika kuvifanya ni pamoja na kumjengea nyumba mama wa binti huyu.

Chanzo cha karibu kimeeleza kuwa Weasel ana mapenzi ya dhati kwa binti huyu ikiwa ni ndoto yake kubwa kuwa nae katika maisha ya familia na kuwa baba bora kabisa.

Muimbaji huyu amekuwa akituhumiwa kuwa na watoto wengi hali iliyopelekea kugombana na mpenzi wake kufikia hatua ya kutozungumza kabisa lakini baadae walipokaa pamoja na kuyazungumza ndipo mschana huyo akatoa hitaji lake la mama yake kujengewa nyumba.

Inaaminika kwamba kufuatia mapenzi ya dhati ya Weasel kwa samira yupo radhi kufanya lolote kukamilisha ndoto zake

Comments are closed.