WENGER AGOMA KUMJIBU MOURINHO

WENGER AGOMA KUMJIBU MOURINHO

Like
246
0
Tuesday, 29 September 2015
Slider

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger  amekataa kujibu chokochoko za Jose Jose Mourinho na kuonyesha zaidi kuwa na malengo na klabu yake.

Mourinho alitoa maneno ambayo kimsingi hayakumtaja Wenger moja kwa moja ila kwa tafsiri ya ndani inaonyesha meneja huyu wa Chelsea alilenga kumsema Arsene Wenger.

katika maelezo yake Mourinho alitaja kufanana kwa waalimu wa timu zote zinazoshiriki ligi ya Uingereza kuwa na presha ya kutotaka kufanya vibaya hali inayowafanya wawe na kazi ngumu katika kuhakikisha wanafikia malengo huku akiwataja waalimu kama Steve [McClaren], [Manuel] Pellegrini, Brendan [Rodgers].

Lakini Mourinho amedai kuwa yupo mmoja ambae hajamtaja kwenye orodha kuwa ni mtu asiyejari na ni mtu mwenye kuweza kuwazungumzia waamuzi kabla ya mchezo, hana mafanikio lakini bado anakaa kama mfalme alisema Mourinho

 

Akihojiwa kwa upande wake Arsene Wenger mara baada ya ushindi wa klabu yake wa magoli 5-2 dhidi ya Leicester City siku ya jumamosi wenger amesema hakuona mtazamo wa Mourinho kama ulimlenga yeye

Wenger amesema anajisikia vizuri kufanya kazi yake kwa timu na mashabiki wake kwa kupata ushindi.

Comments are closed.