WEWE NDIO MCHIZI WANGU.

WEWE NDIO MCHIZI WANGU.

Like
906
0
Friday, 13 February 2015
Entertanment

 

Kila mwaka,tarehe 14 Februari,watu duniani kote huadhimisha siku ya wapendanao duniani.

Kama ilivyo ada,wengi wetu tumezoea kuadhimisha siku hiyo na aidha mume,mke au mpenzi.

Ila kituo cha redio cha 93.7 EFM, kinawapa nafasi ya kipekee wasikilizaji wao kuchagua mtu ambao wao ndio wanamuona kama mchizi wao.

Meneja Uhusiano wa 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole,amesema mchizi wako sio lazima awe mpenzi wako,bali anaweza kuwa kaka,dada,jirani,bosi wako au hata mama mkwe wako,wote hao wanaweza kuwa mchizi wako.

“Sio lazima kila mwaka tufanye mambo yale yale,tumeona tufanye mabadiliko kidogo,alisemea meneja huyo.

Siku ya “wewe ndio mchizi wangu”,itafanyika pale Msasani Beach Club,siku ya tarehe 14 mwezi huu wa February mwaka 2015,ambapo itahusisha wasanii kama vile Mesen Selecta (Mzee wa kanya boya),Recho Kizunguzungu,Msaga sumu,Snura, Sir Juma Nature,RDJ Majay akiwa na Zungu the drama na wengine kibao.

Kanky alisema kwamba ukija na mchizi wako,kutakuwa na zawadi kubwa sana kutoka kwa DJ Majay na Zungu the drama.

“Tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi,kwani watangazaji wote watakuja kupiga picha na kuongea na mchizi wa EFM 93.7.Bado tunaendelea kuwaleta wasikilizaji wetu karibu na sisi,kama mnakumbuka mwaka jana,tuliwaletea tamasha la “Mziki Mnene”,ambapo tulipata nasafi kubwa ya kujumuika na washabiki wetu kwa mda wa miezi mitatu mfululizo,na tukawaahidi kuwaletea mambo mengi mbele ya macho yao”,alisema meneja uhusiano huyo.

Kanky alisema kuwa,zawadi nyingi zitatolewa kwa mtu na mchizi wake na pia kutakua na michezo mbali mbali ambayo itafanyika siku hiyo ya 14 February 2015.

Aliendelea na kusema kwamba hii sio tamasha bali watu waje na machizi wao kuja kuchizika,ni kuanzia saa kumi jioni mpaka watakapo choka.

1

 Team Nzima ambayo inaongoza kipindi cha ya sports headquaters ambacho kinaruka kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa saa tatu mpaka saa sita mchana(Kweli wamechizika).
2
RDJ X5 kutoka EFM akiwa na mchizi wake Kingwendu.
3
JimmyJam,mmoja wa producers hatari wa hapa EFM  akiwa na mchizi wake Jo-Gift.
4
Kala Pina akiweka pozi la nguvu na mchizi wake Swebe.Unaweza kumsikiliza Swebe katika kipindi cha Gurudumu ambacho kinarushwa kila siku Jumatatu mpaka Ijumaa Saa Sita mchana mpaka saa Tisa,akiwa na mwanadada Safia,Manganje pamoja na RDJ X5.
5
Meneja Uhusiano wa EFM Kanky Mwaigomole akiwa na mchizi wake Samira Kiango.Samira ni mhariri msaidizi katika chumba cha habari cha EFM Redio na pia ni mtangazaji wa habari.
6
Scholastica Mazula akiwa na mchizi wake Brighton.Scholastica ni mhariri mkuu wa chumba cha habari cha EFM redio,na pia ni muongozaji wa kIpindi cha Mezani kinachorushwa kila siku ya Jumamosi saa mbili asubuhi mpaka saa nne.
7
Francis Mhando ni mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Sports Headquaters akiwang’ara na machizi wake kutoka Canada.
IMAG0194
Kushoto ni Rachel mtangazaji wa kipindi cha joto la asubuhi akiwa na mchizi wake
IMG_5421
Kulia ni Asha Manga kutoka kipindi cha gurudumu  pamoja na mchizi wake
WP_20150203_11_45_51_Raw

Kushoto ni Geofrey akiwa na mchizi wake

IMG-20150213-WA0002

Marry Bosa akiwa na mchizi wake

IMG_20150213_123115

 

Aunt Fifi akiwa na mchizi wake ONE B

20150213_123500

Aisha Mbegu na mchizi wake

IMG-20150213-WA0003

Comments are closed.