WHO: EBOLA YAANGAMIZWA NIGERIA

WHO: EBOLA YAANGAMIZWA NIGERIA

Like
330
0
Monday, 20 October 2014
Global News

Shirika la afya duniani linatarajiwa kutangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa bola baadae hii leo, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo .

Nchi giyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, alipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai.

Shirika la afya duniani lilitangaza Senegal kutokuwa tena na Ebola mnamo siku ya Ijumaa.

Mlipuko unaoshuhudiwa wa Ebola, umewaua watu 4,500 katika kanda ya Afrika Magharibi hasa nchini Liberia , Guinea na Sierra Leone.

Inakisiwa 70% ya wale walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki katika mataifa hayo.

WHO

Shirika la afya duniani linaweza tu kutangaza nchi kutokuwa na Ebola ikiwa siku 21 zitapita bila ya kuripotiwa kwa visa vipya vya Ebola.

Kisa cha mwisho kilichoripotiwa cha maambukizi mapya ya Ebola, kiliripotiwa tarehe 5 Septemba.

Janga hilo, lilianza kuripotiwa,wakati raia mmoja wa Liberia kuripotiwa kuwa na Ebola mwezi Julai.

Nigeria ilitangaza hali ya tahadhari kiafya huku bwana Sawyer akifariki baadaye kutokana na ugonjwa huo pamoja na raia wengine saba wa Nigeria.

Raia hao walikuwa pamoja na Daktari Ameyo Stella Adadevoh, aliyetambua kuwa Sawyer alikuwa na Ebola na alisifika kwa kusaidia katika harakati za kudhibiti ugonjwa huo.

Balozi wa Liberia alipeleka virusi vya ebola mjini Lagos mwezi Julai.

Alikuguliwa kuwa na Ebola hospitalini alipofanyiwa uchunguzi wa awali .

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Daktari Benjamin Ohiaeri, amesema kuwa mlipuko huo umekuwa na athari kubwa.

Mawaziri mambo ya nje wa muungano wa ulaya wanakutana hii leo kujadili mikakati ya kudhibiti maambukizi ya ebola .

Zaidi ya watu 4500 wamekufa kutokanma na mlipuko wa ugonjwa huo wengi wao raia wa Afrika Magharibi .

 

Comments are closed.