SHIRIKA LA AFYA Duniani -WHO limesema idadi ya vifo vilivyotokana na mripuko wa ugonjwa wa maradhi ya Ebola Afrika magharibi imeongezeka na kufikia 7,842 kati ya kesi 20,081 zilizorekodiwa.
Idadi ya mwisho ya vifo ilikuwa ni 7,693 na kesi 19,695 taarifa za Ebola zilizotolewa Desember mwaka huu.
Takriban vifo na kesi zote za ugonjwa wa wa maradhi ya Ebola zimerekodiwa katika nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zimeathiriwa zaidi na mripuko huo yaani Sierra Leone, Liberia na Guinea.