WHO: IDADI YA WALIOKUFA KWA EBOLA YAONGEZEKA, CHANJO YALETA MATUMAINI

WHO: IDADI YA WALIOKUFA KWA EBOLA YAONGEZEKA, CHANJO YALETA MATUMAINI

Like
381
0
Thursday, 27 November 2014
Global News

SHIRIKA la afya la Kimataifa WHO, limesema idadi ya waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola imeongezeka na kufikia watu 5689.

Jumla ya watu 16, 000 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo  katika nchi nne-shirika hilo la Umoja wa mataifa linasema.

Mataifa matatu ya Afrika Magharibi, Guinea, Sierra Leone na Liberia ndio yaliyoathirika zaidi na maradhi hayo.

Katika hatua nyingine Watafiti wa chanjo ya Ebola nchini Marekani wamesema kuwa wametiwa moyo na matokeo ya awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo.

 

 

Comments are closed.