WHO KUITANGAZA GUINEA NCHI ISIYO NA EBOLA

WHO KUITANGAZA GUINEA NCHI ISIYO NA EBOLA

Like
198
0
Tuesday, 29 December 2015
Global News

SHIRIKA la Afya Duniani leo linatarajiwa kuitangaza Guinea kuwa nchi isiyo na maambukizo ya ugonjwa wa Ebola.

Mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Ebola ulianza nchini humo miaka miwili iliyopita.

Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi za Afrika magharibi, hususan katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Waguinea wanajiandaa kusherehekea kumalizika kwa janga hilo nchini mwao kwa kufanya maonesho na kurusha fataki.

Comments are closed.