WHO LAHIMIZA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA ZIKA KUCHUKUA TAHADHARI

WHO LAHIMIZA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA ZIKA KUCHUKUA TAHADHARI

Like
267
0
Tuesday, 31 May 2016
Global News

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limewahimiza watu wanaotoka katika sehemu zilizoathirika na virusi vya Zika kuzingatia mbinu za kujikinga endapo mtu anafanya mapenzi au kujiepusha na ngono kwa muda wa wiki nane.

WHO imeongeza kwamba ni muhimu kwa wanawake kuepuka kupata ujauzito kwa miezi sita iwapo mwenzake wa ndoa amekuwa na dalili za virusi vya ugonjwa huo.

Wiki iliyopita shirika hilo lilisema kuwa hakuna sababu ya kujiepusha na michezo ya Olimpiki mjini Rio mwezi Agosti.

Comments are closed.